Monday, 9 September 2013
Mimi kabla ya kufika hili eneo liitwalo nyamongo nimekuwa nikiskia matukio mbalimbali kutoka katika eneo hili,mengi ni ya kutisha hasa namna uendeshwaji wa mgodi wa north mara ulivyo na athali katika maeneo ambayo yameuzunguka.suala la kwanza ni udhibiti mbovu wa maji machafu yenye mchanganyiko wa sumu.kweli lambo lipo lakini mfumo waujenzi wa hilo bwawa ni hafifu kwa sababu ni mawe yamewekwa,blanket ambalo ukilimwagia maji yanapenya pamoja na udongo mita 5 kutoka kwenye blanket,kizuizi pekee cha haya maji ni udongo na kibaya zaidi hili bwawa limepanda juu zaidi ya mita 40.Eneo la matongo kuna pump,kegonga kuna pump na two-six jirani na kwimange pump ipo na zote hufanya kazi ya kurudisha maji yalovuja kutoka lamboni, maji huwa mengi na kuzidia hizi pump(matongo na kegonga) hasa mvua inaponyesha,lakin kwimange yani ni mto kabisa na watu wanaoga pasipo kujua kwamba yale maji ni mchanganyiko wa ammonium na kemikali nyingine za orica pamoja na kemikali hatari zaidi kutoka plant.katika maeneo haya matatu mifugo hawatamaniki,wamekonda xana japo nyasi zipo za kutosha.Lazima tuelezane na inapobidi kueleweshana kwamba mstakabali wa maisha yetu sisi kama watanzania ni upi,kwa sababu kama jambo linaonekana wazi halafu linafumbiwa macho na watu wanazidi kuathirika ni dhahili kwamba serikali haiwajibiki hata kidogo kuwalinda raia wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment